Sir Alex Ferguson amekiri waziwazi kuwa maamuzi yake ya kutangaza kuwa angestaafu mwaka 2001 lilikuwa ni kosa kubwa katika maisha yake ya ukocha.
Kocha huyo wa zamani wa Man Utd Sir Alex Ferguson alikaa klabuni hapo kwa miaka 15 ndipo alipotangaza kuwa ataondoka klabuni hapo baada ya msimu mmoja mbele.
Lakini miezi 6 baadae Fergie aligundua kuwa alifanya kosa na akakubali kubaki Old Trafford.
“Kosa kubwa nililowahi kufanya nikiwa Manchester United ni kutangaza kuwa nitaachana na Man Utd mwanzo wa msimu” alisema Fergie akiiambia Daily Mirror.
“Nafikiri hicho kitu kiliwakatisha tama watu wengi, kujua Ooh! Kumbe kocha anaondoka, lakini nilipobadili maamuzi yangu mwezi January, nilianza kuifikiria tena United na ni kwa jinsi gani tungepambana kumaliza katika nafasi za juu” aliongeza Ferguson.
Ferguson alikiri kuwa familia yake na viongozi wa timu walichangia katika kubadilisha maamuzi yake ya kustaafu ukocha na kuendele kubaki kuitumikia klabu hiyo.
alisema “Ni kitu kizuri kusikiliza ushauri wa viongozi na wafanyakazi wenzio”
“Mwaka 2005, kipindi hicho hatukufanikiwa kushinda taji lolote, wakati huo ambapo kabla nilitangaza kustaafu kuitumikia klabu na hicho kitu ndo kiliwaathiri wachezaji na watu wote”
“Lilikuwa ni kosa na mke wangu pamoja na watoto wangu 4 walisaidi kubadili mtazamo wangu, na nilianza kufikiri tena, baada ya hapo ndipo Wayne Rooney na Christiano Ronaldo wakajiunga na klabu na tukaanza kurudisha morali ya wachezaji na klabu”
Ferguson aliendelea kusema baada ya kujutia kosa lake hilo na kuamua kubaki katika klabu na mara baada ya Rooney na Ronaldo kuongeza nguvu katika kikosi cha United ndipo mambo yalibadilika na kuanza kushinda mataji ya ligi mara nyingi zaidi.
United inamaliza mechi zake za ligi jumapili hii katika uwanja wa Old Trafford dhidi ya Bournemouth, na baada ya hapo wataenda Wembley kucheza na Crystal Palace katika fainali ya FA Cup.
0 comments:
Post a Comment