Msimu wa ligi wa 2015/16 umekuwa msimu mbaya kwa wakazi wa jiji la Stuttgart katika tasnia ya mpira wa miguu. Timu tatu za Stuttgart zimeshuka daraja katika ligi zote 3 zikizoshiriki, Stuttgart iliyokuwa inashiriki ligi kuu kwa maana Bundesliga, Stuttgart II ya ligi daraja la kwanza na Stuttgarter Kickers waliokuwa katika ligi daraja la pili.
Timu hizo zote zimejikuta zikishuka daraja katika ligi walizokuwa wanashiriki, Stuttgart iliyokuwa katika ligi kuu wameshuka daraja rasmi baada ya mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu waliokubali kipigo cha magoli 3 – 1, mabingwa hao wa Bundesliga msimu wa 2007 wameshuka daraja baada ya kudumu katika ligi kuu kwa takribani miaka 39 bila kushuka daraja.
Stuttgart II tayari wao walishashuka daraja hata kabla ya mchezo wao wa mwisho na Stuttgarter Kickers wao wameshuka daraja baada ya kukubali kichapo katika uwanja wao wa nyumbani cha goli 1 – 0 kutoka kwa Cheminitzer FC .
0 comments:
Post a Comment