Friday, May 27, 2016

RICARDO KAKA AITWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA BRAZIL

Ricardo Izecson dos Santos Leite Maarufu kama Kaka ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kuchukua nafasi ya Staa wa Bayern Munich Douglas Costa katika michuano ya Copa America


Shirikisho la mpira wa miguu Brazil limethibitisha kuwa Winga wa Bayern Munich Douglas Costa ataikosa michuano ya Copa America na nafasi yake kuzibwa na Kaka.
Costa 25, anamaumivu ya misuli katika mguu wake wa kushoto kitu kinachomuweka nje katika michuano hiyo.

Mashabiki ambao walimiss vitu vya kaka sasa ni wakati wao kumuona tena akiitumikia tena timu yake ya taifa.

0 comments:

Post a Comment