Tuesday, May 24, 2016

FIFA YAMTIMUA MKURUGENZI WA FEDHA

FIFA imemtimua mkurugenzi wake wa masuala ya fedha aliyedumu katika shirikisho hilo kwa zaidi ya miaka 12.

Markus Kattner



Markus Kattner ametimuliwa kufuatia kashifa yake ya  kupokea fedha za ziada ambazo zilikuwa ni kinyume na utaratibu, kutimuliwa kwa Markus kuomeonekana ni kusafisha kabisa masalia ya Sepp Blatter katika Shirikisho hilo.

FIFA wamesema Kattner amefukuzwa baada ya uchunguzi wa ndani kuthibitisha kuwa alivunja sheria ya majukumu ya shirikisho hilo kunakohusishwa pia na mkataba wake wa ajira. Kattner alituhumiwa kupokea mamilioni ya dola alizokuwa akijiongezea katika mkataba wake kinyume na utaratibu. Malipo hayo ya ziada yalikuwa yanajulikana na Blatter na katibu mkuu Jerome Valcke lakini hawakuchukua hatua yoyote.

"Hatujajua bado kwanini haya malipo yalifanyika" alisema mtu wa FIFA ambae hakutaka jina lake kutajwa kwa sababu za kiuchunguzi, "Mikataba ya namna hii haikuwa inajulikana wazi na ilikuwa haijulikani pia kwa Maafisa sahihi wa FIFA" aliongeza.

Kattner alikuwa katika makao makuu ya FIFA jumatatu kabla kutimuliwa kwake hakujatangazwa. FIFA ilishawahi kusema kuwa malipo hayo yalikuwa yanajulikana pia na aliyekuwa mwenyekiti wa muda mrefu wa kamati ya fedha bwana Julio Grondona raia wa Argentina, Grondona alifariki mwaka 2014

0 comments:

Post a Comment