Monday, May 30, 2016

NAIBU WA CHAMA CHA KUPAMBANA NA UHAMIAJI UJERUMANI AMTOLEA MANENO YA KIBAGUZI JEROME BOATENG

Naibu Kiongozi wa Chama Cha kupambana na Uhamiaji Ujerumani ameonyesha wazi ubaguzi wake kwa Jerome Boateng mchezaji wa Bayern na Timu ya Taifa ya Ujerumani. 

Alexander Gauland



Alexander Gauland, alisema watu wanafikiri Boateng ni mchezaji mzuri lakini kamwe yeye hawezi kumfanya rafiki, Gauland alizungumza maneno hayo alipokuwa anazungumza na gazeti la Ujerumani la The Frankfurter Allgemeine.  


Kitendo hicho kimemfanya naibu huyo alaaniwe vikali na wachezaji mbalimbali, Rais wa shirikisho la soka Ujerumani pamoja na waziri wa mambo ya Ndani. 

Hata hivyo Gauland alijibu baadae kuwa hakumaanisha kumdhalilisha Jerome Boateng.

0 comments:

Post a Comment