Timu ya soka ya Simba SC imejikuta nje ya michuano ya FA baada ya kupokea kichapo toka kwa timu ya Coastal Union.
Katika mchezo huo wa vuta nikuvute Coasta ilikuwa yakwanza kutikisa nyavu za Simba baada ya mchezaji Yusuf kupiga mpira wa adhabu ambao ulitinga moja kwamoja nyavuni na kumwacha mlinda mlango wa Simba akiwa ameshika kiuno pasipo kujua lakufanya.
Mpaka timu zinakwenda mapumziko, Coastal ilikuwa ikiongoza kwa Goli 1 - 0
Kipindi chapili kilianza kwa kasi ambapo timu ya soka ya Simba ilifanya mashambulizi ya mara kwamara langoni mwa coastal ambapo katika dakika ya 49 mshambuliaji Kiiza alifanikiwa kusawazisha goli na kufanya ubao wa matangazo usomeke 1-1
Mnamo dakika ya 82 mcezaji wa Coastal union alifanyiwa madhambi na mlinzi wa Simba jambo lililopelekea Coastal kupata penati na kupachika bao lapili na la ushindi.
Kwamatokeo haya, Simba inatupwa nje ya michuano ya FA na endapo haitachukua ubingwa wa bara haitashiriki kwa mara nyingine katika michuano ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment