Monday, May 30, 2016

JULIO NA NDOTO ZA UBINGWA WA LIGI KUU MSIMU UJAO

Kocha wa timu ya Mwadui FC, Jamhuri Kiwelu Julio anaamini ubingwa unawezekana katika msimu ujao wa ligi.





Julio amesema anajipanga vizuri kukiweka kikosi chake sawa ili waweze kutwaa ubingwa wa ligi msimu ujao. Kitendo cha Mwadui FC kumaliza katika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi kuu msimu wa 2015/16 kumemfanya Julio aamini kuwa timu yake inaweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu ujao.

Mwadui ambayo imeshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu imeonyesha ushindani mkubwa katika ligi kwa timu zote ndogo na kubwa.

"Kama tumeweza kumaliza nafasi ya sita kwenye msimu wa kwanza basi hata ubingwa unawezekana kwa sababu ukiangalia tuliweza kucheza vizuri dhidi ya timu kubwa za Yanga, Azam na Simba na kufika nusu fainali ya Kombe la FA" alisema Julio akionyesha imani yake kubwa ya kutwaa ubingwa msimu ujao.

Julio aliongeza kuwa kikubwa  ni kufanya usajili wa uhakika wa wachezaji wenye uwezo mkubwa.

0 comments:

Post a Comment