Monday, May 30, 2016

NGASA ANARUDI YANGA

Mrisho Halfan Ngassa Mtanzania anayecheza katika klabu ya Free State ya Nchini Afrika Kusini amesema yupo tayari kurudi kucheza Yanga.



Winga huyo wa Kimataifa raia wa Tanzania anacheza katika klabu ya Free State inayoshiriki Ligi kuu nchini Afrika Kusini PSL.

Alipozungumza na Goal Ngasa amesema yupo tayari kurudi Yanga ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho hata kwa mkopo.

"Nipo nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi lakini nimekutana na viongozi Pamoja na kocha Hans Van der Pluijm, Wameonyesha nia ya kunihitaji katika hatua ya makundi na mimi nipo tayari kurejea nyumbani ila itakuwa vizuri kama wataongea na uongozi wa timu yangu Free State." alisema Mrisho Ngasa.

Yanga ambayo ipo katika hatua za mwisho za maandalizi kabla hatua ya makundi kombe la shririkisho barani Afrika haijaanza kutimua vumbi, wanahitaji kuimarisha kikosi chao kwa kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa kucheza michuano ya kimataifa ili kuweza kuleta ushindani kwa wapinzani katika hatua hiyo.

0 comments:

Post a Comment