Saturday, August 6, 2016

YALIYOJIRI MKUTANO MKUU WA DHARULA YANGA

Katika mkutano mkuu wa dharula wa klabu ya Yanga uliofanyika leo ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti Yusuf Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.

Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini ya Manji. 

Aidha, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu, Francis Kifukwe alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo, wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji.

Wajumbe watatu wa kamati ya utendaji Hashim Abdallah, Ayoub Nyenzi na Salum Mkemi wamefukuzwa na kufutiwa uanachama kutokana na kutokuwa waaminifu kufanya mambo kinyume na katiba ya klabu ya Yanga.

Kabla ya wajumbe hao kufutiwa uanachama Manji aliuliza mara 3 wanachama waliokuwepo kama wanaweza kuwatetea ama kuwapigia kura waendelee kuwa sehemu ya familia ya Yanga lakini hakuna mwanachama aliyejitokeza.
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA


0 comments:

Post a Comment