Thursday, May 5, 2016

UJUMBE WA JURGEN KLOPP KWA MASHABIKI WA LIVERPOOL





KLABU Ya Liverpool leo itawakaribisha Villarreal kutoka Nchini Hispania katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Uefa Europa League utakaopigwa katika dimba la Anfield, saa 4:05 usiku wa leo.

Katika Mchezo wa kwanza Liverpool ilikubali kichapo cha goli 1 - 0, hivyo leo kulazimika kupata ushindi wa goli 2 - 0 ili waweze kusonga mbele.
kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema  "Hebu tuonyeshe sura yetu ya kweli, mood yetu ya kweli, mtazamo wetu na hebu tuonyeshe uwezo wetu bora juu ya klabu hii ya ajabu " akiwahamasisha mashabiki pamoja na wachezaji kufanya kweli katika mchezo wao wa leo dhidi ya Villarreal.
Liverpool ilitinga katika hatua hii ya nusu fainali baada ya kuiondosha Dortmund ya nchini Ujerumani.

0 comments:

Post a Comment