Saturday, June 4, 2016

CAMEROON YAFUZU FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Timu ya taifa ya Cameroon imefanikiwa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika baada ya kupata ushindi wa ugenini wa goli 1 - 0 dhidi ya Mauritania.


Ushindi wa goli 1 - 0 umetosha kuipeleka Cameroon katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazochezwa nchini Gabon mwaka 2017. Cameroon ilipata ushindi huo kufuatia bao alilofunga Winga wa kikosi hicho Edgar Salli katika dakika ya 31 ya mchezo.

Wakati Cameroon wakifurahia ushindi huo, timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana mambo yameonekana kuwa si mazuri kwa upande wao baada ya kutolewa kufuatia matokeo hayo ya Cameroon na sasa watacheza mchezo wao na Gambia ikiwa tu ni kukamilisha ratiba katika kundi lao.

Timu ambazo tayari zimefuzu kucheza fainali hizo ni;

Gabon - Wenyeji wa mashindano hayo
Algeria na 
Morocco.

0 comments:

Post a Comment