Wednesday, March 8, 2017

Barcelona vs PSG, je Barcelona kushinda 5 - 0 ?


Muda: 22:45
Barcelona wanaikaribisha PSG katika dimba la Camp Nou wakiwa na kumbukumbu ya kipigo kikali cha goli 4 – 0 walichokipata February 14  mwaka huu.
Barcelona ndio vinara wa ligi kuu ya Hispania kwa kujikusanyia pointi 60 baada ya michezo 26 mbele ya real Madrid wenye pointi 59 baada ya michezo 25.
Baada ya kichapo hicho Barcelona wanaonekana kujipanga upya na wamekuwa wakipata ushindi mkubwa hasa katika michezo yao ya mwisho angalia rekodi hapo chini za laliga.
MICHEZO 5 YAMWISHO YA BARCELONA
Barcelona 5-0 Celta Vigo Mar 4, 2017   LALIGA
Barcelona 6-1 Sporting Gijón Mar 1, 2017        LALIGA
Atletico Madrid 1-2 Barcelona Feb 26, 2017       LALIGA
Barcelona 2-1 Leganes Feb 19, 2017          LALIGA
Paris Saint-Germain 4-0 Barcelona Feb 14, 2017 UEFA Champions League
PSG tangu waifunge Barcelona hawajapoteza mchezo, wameshinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja, Miongoni mwa michezo hiyo ni ushindi mkubwa kabisa wa goli 5 – 1 ugenini dhidi ya Marseille kwenye ligi kuu ya Ufaransa.
Tizama Matokeo ya PSG kwenye michezo yake mitano ya mwisho .
MICHEZO 5 YA MWISHO YA PSG
Paris Saint-Germain 1-0 AS Nancy, Mar 4, 2017 Ligue 1
Niort 0-2 Paris Saint-Germain Mar 1, 2017 LIGI
Marseille 1-5 Paris Saint-Germain Feb 26, 2017 Ligue 1
Paris Saint-Germain 0-0 Toulouse Feb 19, 2017  Ligue 1
Paris Saint-Germain 4-0 Barcelona Feb 14, 2017 UEFA Champions League
MICHEZO 5YA MWISHO  WALIYOKUTANA  (Head To Head Record
)
Katika michezo mitano iliyozikutanisha timu hizi mbili Barcelona imeshinda mara tatu na PSG wameshinda mara mbili. Angalia Matokeo hapa chini.
Paris Saint-Germain 4-0 Barcelona Feb 14, 2017 UEFA Champions League
Barcelona 2-0 Paris Saint-Germain Apr 21, 2015 UEFA Champions League
Paris Saint-Germain 1-3 Barcelona Apr 15, 2015 UEFA Champions League
Barcelona 3-1 Paris Saint-Germain Dec 10, 2014 UEFA Champions League
Paris Saint-Germain 3-2 Barcelona Sep 30, 2014 UEFA Champions League
Je kwa mtiririko  huo hapo juu Barcelona itaweza kuifunga PSG goli 5 – 0 ?.
Je PSG haitapata goli Camp Nou leo?

Toa maoni yako 

0 comments:

Post a Comment