Marouane Fallaini ameweka wazi kuwa Kocha Jose Mourinho alimtumia ujumbe alipowasili Man United.
Kiungo huyo wa Ubelgiji amesema Mourinho alimtumia ujumbe akimkaribisha United huku pia akimtakia kila la kheri katika michuano ya Euro
"Mourinho aliwasiliana na mimi kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS), akinikaribisha United na kunitakia Euro njema" alisema Fellaini alipokuwa katika mazoezi ya timu yake ya taifa jana jumamosi.
Fellaini alisema amefurahishwa na ujio wa kocha Mourinho klabuni United na kwamba yupo tayari kufanya kazi chini ya kocha huyo.
"Anapenda kushinda mataji na itakuwa ni heshima kubwa kwangu kufanya kazi na yeye. Sasa kazi ipo kwangu kumfanya aniamini na kunipanga kikosi cha kwanza" aliongeeza Fellaini.
Ujio wa Mourinho Man Utd umepokelewa kwa hisia tofauti na wachezaji wa klabu hiyo, kwani wapo ambao kuchukua kwake mikoba klabuni hapo ndio kunahitimisha uwepo wao United huku wengine wakifurahia baada ya kuhakikishiwa kuendelea kuwepo klabuni hapo.
Wachezaji ambao tayari Mourinho ameshaonyesha kutokuwahitaji klabuni Hapo ni Daley Blind, pamoja na Nick Powell na huenda idadi hiyo ikaongezeka.
==============
Bonyeza hapa ku-Like Page yetu ya Facebook
==============
0 comments:
Post a Comment