Saturday, June 18, 2016

KIPAUMBELE NAMBA 1 CHA SIMBA KATIKA USAJILI HIKI

Simba ipo katika harakati za kuimarisha kikosi chao kwa kuhakikisha hawafanyi makosa katika usajili kipindi hiki ambacho dirisha la usajili limefunguliwa.

Uongozi wa Simba umesema kipaumbele chao cha kwanza katika kipindi hiki cha usajili ni kocha, wanataka wampate kocha mwenye rekodi nzuri ambaye pia atawasaidia katika kuwasajili wachezaji wazuri, Mwenyekiti wa klabu hiyo Evans Aveva amebainisha hilo kwa kusema lengo ni kushirikiana na kocha huyo katika kufanya usajili ambao utakuwa ni wa uhakika.

"tunaona suala la kocha liwe namba moja, wachezaji tayari tumeanza kusajili vizuri lakini itapendeza kama tutakuwa na ushirikiano wa karibu na mkuu wa benchi la ufundi maana wao ndiyo wataalamu zaidi yetu." alisema Aveva.

Bosi wa kamati ya usajili Zacharia Hans Poppe alisafiri kwenda nchini Zimbabwe kujaribu kuzungumza na kocha anayeifundisha timu ya taifa ya Zimbabwe, Kalisto Pasuwa lakini juhudi hizo ziligonga mwamba na kumkosa kocha na kuamaua kuongeza kasi za kusaka kocha mwingine.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Related Posts:

  • KIKOSI CHA YANGA LEO DHIDI YA TOTO AFRICANS KIKOSI CHA YANGA LEO. 1. Deogratius Munishi Dida. 2. Juma Abdul Japhary. 3. Oscar Fanuel Joshua. 4. Kelvin Patrick Yondani. 5. Vicent Bossou. 6. Salum Abo Telela. 7. Saimon Happygod Msuva. 8. Haruna Fadhil Niyo… Read More
  • TCHETCHE YUKO FITI KUIVAA SIMBA MSHAMBULIAJI hatari wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Kipre Tchetche, yupo fiti asilimia 100 kuivaa Simba  kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Taifa, D… Read More
  • Dennis Kitambi Aeleza Siri Ya Ushindi Wao Dhidi Ya Majimaji KOCHA Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Dennis Kitambi, amesema kuwa maelekezo waliyowapa wachezaji wao ya kuongeza hali ya kupambana mchezoni kabla ya kuanza kipindi cha pili ndio yamepelekea… Read More
  • YANGA YAENDELEA KUJIWEKA FITI KLABU ya Dar Young Africans imeendelea na mazoezi huko mwanza katika viwanja vya DIT wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Toto Africans ambao utachezwa siku ya Jumamosi April 30, Yanga ambayo inashika nafasi ya kwanza kw… Read More
  • SIMBA WAREJEA DAR TAYARI KWA KUIVAA AZAM FC TIMU ya Simba Sports Club imewasili jijini Dar wakitokea visiwani Zanzibar ambako walikwenda kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC. Simba inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi inahitaji ushindi katika mchez… Read More

0 comments:

Post a Comment