Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, Poppe amesema lazima Yanga wawapatie Simba kiasi cha pesa ndipo waandike barua ya kumtumia mchezaji huyo.
Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kwamba wanafanya hivo kwa kuwa kipindi cha kuidhinisha usajili kwa Tanzania bara bado hakijafika, hivyo njia pekee ya Yanga kuweza kumtumia Hassan Ramadhan ni hadi Simba iandike barua ya kumruhusu mchezaji huyo kutoka katika klabu ya Simba timu yake ya Zamani.
"Tunasubiri pesa kutoka kwa Yanga ili tuweze kuandika barua ya kumruhusu Kessy kucheza mechi zao za kombe la shirikisho, vinginevyo hatuta mruhusu hadi hapo usajili utakapopitishwa" alisema Hans Pope.
Kwa upande wao Yanga wamesema hawatotoa kiasi chochote cha pesa kwa Simba na kama wao hawataki kuandika hiyo barua basi watasubiri hadi hapo usajili utakapoidhinishwa.
Yanga walishindwa kuwatumia wachezaji wake wapya kutokana na kutokuwa na barua kutoka kwenye timu zao za zamani.
0 comments:
Post a Comment