Thursday, May 5, 2016

BREAKING NEWS: AZAM FC YAPOKWA POINTI 3 NA MAGOLI 3


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema katika mechi namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Azam ilimchezesha Nyoni kinyume na sheria huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine dhidi ya Mbeya City, Azam FC ilishinda 3-0. Kufuatia maamuzi ya TFF, Mbeya City imepewa points 3 na magoli 3.

“Azam wamepoteza mchezo ule na sasa Mbeya City imepewa pointi tatu na mabao matatu pia tumelipa onyo benchi la ufundi la Azam kuwa makini ili jambo hili lisiwatokee tena,” alisema Lucas.

0 comments:

Post a Comment