Thursday, May 5, 2016

FARID MUSSA AFUZU MAJARIBIO HUKO NCHINI HISPANIA


Mchezaji wa Azam FC Farid Mussa aliye nchini Hispania alikokwenda kwa lengo la kufanya majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza, amefanikiwa kufuzu majaribio hayo na sasa Uongozi wa klabu hiyo utakaa mezani na Azam FC ili kukamilisha usajili wake.

“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Yusuf Bakhresa Mkurugenzi wa Azam FC.

Faridi ambaye wakati anaondoka nchini alitegemewa kwenda kufanya majaribio katika klabu za Las Palmas na Athletic Club zinazoshiriki ligi kuu Nchini humo maarufu kama La Liga, lakini wakala wake alishauri afanye majaribio katika timu ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza lengo likiwa ni kumwezesha kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ili kuimarisha kipaji chake na kuonekana na klabu kubwa za ligi kuu Nchini humo na Ligi zingine kubwa duniani.

KILA LA KHERI FARID MUSSA

0 comments:

Post a Comment