Friday, May 6, 2016

LIVERPOOL YATINGA FAINALI YAISHUSHIA KIPIGO VILLARREAL


TIMU Ya Liverpool kutoka nchini England jana usiku imefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao waliocheza na Klabu ya Villarreal kutoka Nchini Hispania, Mechi ya pili ya nusu fainali ya Uefa Europa league, iliyochezwa katika uwanja wa Anfield na kuibuka na ushindi wa 3 - 0.

Liverpool walipata goli la kwanza kupitia kwa Bruno dakika ya 7 aliyejifunga baada ya mpira wa krosi uliopigwa na Sturridge kumgonga tumboni na kuzama nyavuni, goli la pili lilifungwa na Daniel Sturridge kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango katika dakika ya 63 na goli la mwisho yani la 3 lilifungwa na Adam Lalana katika dakika ya 81 ya mchezo, Matokeo hayo yameivusha Liverpool katika hatua ya nusu fainali na sasa watacheza fainali na Klabu ya Sevilla ya Nchini Hispania ambayo nayo jana iliibuka na ushindi wa magoli 3 - 1 dhidi ya Shakhtar, ambapo katika mechi ya awali timu hizi zilitoka sare ya 2 - 2, hivyo Sevilla kusonga mbele kwa jumla ya magoli 5 - 3.

Fainali ya Michuano hii itafanyika katika uwanja wa  St. Jakob-Park Jijini Basel huko Nchini Switzerland May 18,2016.


0 comments:

Post a Comment