Friday, May 6, 2016

SEVILLA KUCHEZA FAINALI MARA YA 3 MFULULIZO



KLABU Ya  Sevilla ya Nchini Hispania imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3 - 1 jana katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya kombe la Uefa Europa League ilipocheza na Shakhtar. katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 2 - 2, hivyo kwa matokeo ya jana Sevilla amefuzu kucheza katika hatua ya fainali. Hii inakuwa ni Mara ya 3 mfululizo kwa klabu ya Sevilla kucheza fainali ya UEFA Europa League baada ya kuwa wamecheza fainali ya msimu wa 2013-2014, 2014-2015 na msimu huu wa 2015-2016.

Magoli ya Sevilla katika mchezo huo yalifungwa na Gameiro dakika ya 9 na 47, huku goli la tatu likifungwa na Mariano dakika ya 59, na goli la pekee la Shakhtar limefungwa na Edwardo Da Silva dakika ya 44.


0 comments:

Post a Comment