Klopp ametumikia klabu ya Dortmund kwa miaka saba akiwaletea
mafanikio makubwa klabuni hapo ikiwemo kuifikisha klabu hiyo katika level kubwa za kisoka
barani Ulaya.
Kuondoka kwake mwezi mei kuliacha hisia kubwa za majonzi na
shukrani kubwa kutoka kwa mashabiki wake, mashabiki ambao anaamini kurudi kwake
leo katika uwanja wa Signal Iduna Park kutawakatisha tamaa katika mechi ya robo
fainali ya Europa league.
“Sijui watu wanafikiria nini lakini ninachoweza kusema,
tuliposema kwaheri ilikuwa vizuri, ilipendeza” alisema kocha huyo “Najua watu
wengi watafurahi kuniona tena lakini sidhani kama huu ni muda nzuri wa kuonana
na marafiki” aliongeza Jurgen Klopp.
“Nitashangilia kama Liverpool wakifunga goli, nilifanya
hivyo nilipocheza na klabu yangu ya zamani ya Mainz ilipokutana na Dortmund na
nimekaa Mainz kwa miaka 18, kama goli likipatikana dakika za mwanzo sitakimbia
nikishangilia goli hilo lakini ni muhimu kufanya hivyo, sio kwamba napanga
kufanya hivyo hapana lakini pia sitaenda pale nikiwa nimemeza vidonge
vitakavyonizuia kushangilia” alieleza kocha huyo anaeitumika Liverpool kwa
sasa.
Klopp anaiona Dortmund kuwa ni miongoni mwa klabu tano bora
duniani, kikosi cha Dortmund kwa sasa kinaongozwa na wachezaji Pierre-Emerick
Aubameyang, Marco Reus na Henrikh Mkhitaryan
katika safu ya ushambuliaji wakiwa tayari wameshafunga magoli 75 kwa
pamoja, wakati ukichukua idadi ya magoli
ya wachezaji wote wa Liverpool haifikii idadi hiyo iliyofungwa na wachezaji
watatu tu.
Mechi hiyo itapigwa katika dimba la Signal Iduna Park majira
ya saa 4:05 usiku leo.
Mechi zingine za robo
fainali ya Europa leo ni Villarreal vs Sparta, Athletic Club vs Sevilla na
Braga vs Shakhatar D zote zitachezwa muda mmoja
4:05 usiku.
0 comments:
Post a Comment