Thursday, April 7, 2016

SH. MILIONI 220 KUIONDOA AL AHLY KLABU BINGWA AFRIKA

VIINGILIO YANGA V AL AHLY:
VIP A: Sh 30, 000
VIP B: Sh 25, 000
VIP C: Sh 25, 000
Mzunguko: Sh 5,000
(Mchezo utaanza Saa 10:00 jioni Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
Simon Msuva atapata nafasi ya kucheza dhidi ya Al Ahly kwa mara ya pili? 

YANGA inahitaji Sh. Milioni 220 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly nchini Misri Aprili 19.
Yanga watakuwa wenyeji wa Ahly Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 19 mjini Cairo.
Na leo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba wanapaswa kudhibiti mapato ya mchezo wa kwanza Jumamosi ili wapate fedha za maandalizi ya mchezo wa marudiano. 
Amesema fedha hizo zitapatikana kwa kudhibiti mapato ya milangoni, ikiwemo kuzuia kituo chochote cha Televisheni kuonyesha mchezo huo bila makubaliano maalumu.
"Kuna baadhi ya vituo vya Televisheni vya nje vimeomba kurusha matangazo ya mchezo
huo, tuko katika mazungumzo nao, tukikubaliana watarusha,"alisema Muro.
Ameweka wazi kwa hapa nchini hakuna kituo chochote cha Televisheni kitakachoruhusiwa kurusha mchezo huo, zaidi ya vituo vya Redio tu kutangaza.

Related Posts:

  • WASANII, WANAMICHEZO WATENGEWA BILIONI 3 Serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 3 kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ya michezo, sanaa na ubunifu. Pesa hizo zimetengwa na serikali katika mwaka ujao wa fedha,kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa fedha na uchum… Read More
  • YANGA KUANZA KAMBI RASMI LEO Timu ya Dar Young Africans inatarajiwa kuingia kambini leo kujiandaa na michezo ya hatua ya makundi CAF Confederation Cup. Yanga itacheza mchezo wake wa kwanza katika hatua hiyo Juni 19 dhidi ya MO Bejaia ya nchini Algeri… Read More
  • PLUIJM AWACHIMBA MKWARA WACHEZAJI YANGA Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko baada ya fainali ya kombe la shirikisho TFF, Kocha Pluijm ametoa onyo kwa wachezaji wote ambao watachelewa kufika kikosi hapo. Yanga wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa kwa… Read More
  • AARON NYANDA AJIENGUA UCHAGUZI YANGA Nyanda aliyekuwa anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, amejitoa kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika kesho Juni 11, 2016. Nyanda ambaye alichukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwenye ofisi za shirikisho la mpira w… Read More
  • MTIBWA HAITAMBUI USAJILI WA ANDREW VICENT YANGA Klabu ya Yanga hivi karibuni ilitangaza kumnasa mchezaji wa Mtibwa Sugar Andrew Vicent "Dante" lakini Msemaji wa Klabu ya Mtibwa, Thobias Kifaru amesema hana taarifa hizo. Klabu ya Mtibwa Sugar imesema haijapata taarifa j… Read More

0 comments:

Post a Comment