Thursday, April 7, 2016
Hall: Tulishindwa Kutimiza Majukumu Yetu Uwanjani
UKIACHILIA mbali malalamiko ya waamuzi, Kocha Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Stewart Hall, amesema kuwa wameporwa ushindi na Ndanda jana baada ya wachezaji kushindwa kutimiza ipasavyo majukumu yao uwanjani.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 kipindi cha kwanza kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), lakini ilijikuta ikiondoka na pointi moja baada ya Ndanda kusawazisha mabao yote kipindi cha pili.
Mabao ya Azam FC kwenye mchezo huo yalifungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ na Didier Kavumbagu huku Atupele Green akifunga bao la kwanza la Ndanda kwa mkwaju wa penalty na jingine likifungwa na Ahmed Msumi.
Akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz Hall alisema wachezaji walikosa hali ya kujiamini mchezoni na hamu ya kupambana kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo huo.
“Hatukucheza vizuri kabisa, tulicheza vema dakika 20 za mwanzo na baada ya hapo hatukuuonyesha mchezo mzuri hasa kipindi cha pili, nadhani leo (jana) wachezaji walikosa hali ya kujiamini na kutimiza majukumu yao uwanjani. Kila mtu anajisikia furaha kulaumu waamuzi na wengine, lakini wakati huo wachezaji walishindwa kutimiza majukumu yao na hii imeonekana hata kwenye mechi zetu mbili zilizopita.
“Kikosi chetu ni kizuri sana, wachezaji wetu ni wazuri sana, hivyo tunaweza kuwapiga waamuzi na timu zote lakini ili kutimiza hilo lazima tufanye kazi kwa bidii na kujiamini, jambo ambalo tumelikosa leo (jana), kuna baadhi ya makosa ya kiufundi tumefanya, baadhi ya krosi, kona na mipira ya adhabu ndogo tuliyopiga hazikuwa nzuri,” alisema Hall.
Azam FC imefikisha jumla ya pointi 52 na kubakia katika nafasi ya tatu huku ikizidiwa pointi moja na Yanga inayoshika nafasi ya pili na pointi tano dhidi ya Simba iliyo kileleni, lakini imeizidi Yanga mchezo mmoja huku ikizidiwa mechi moja na wekundu hao.
Kikosi cha Azam FC leo saa 2.30 asubuhi kimeanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na mchezo ujao wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance de Tunis utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jumapili ijayo (Aprili 10).
Chanzo: azamfc official site
Related Posts:
Kwa Mchezo Huu Wakimataifa Wajitazame Upya. Ligi ya vodacom imeendelea tena Leo katika viwanja viwili. Mjini Morogoro Mtiwa Sugar waliikalibisha Azam Fc wakati Yanga ikicheza na Mwadui Fc ya Mjini Shinyanga katika uwanja wa taifa. Azam Fc imecheza katika mazingira… Read More
Kiiza, Juuko Murshid Kikaangoni Msimbazi Tayari Simba wameanza kuangushiana lawama za chinichini. Jambo ambalo si sahihi lakini wapo ambao walikuwa chanzo cha kuua umoja katika mechi hiyo au kutokuwa makini, kukachangia wao kung’oka. Kiiza&Juuko kikaangoni:… Read More
Kikosi Cha Yanga Dhidi Ya Mwadui Leo Hiki Hapa KIKOSI CHA YANGA LEO. 1. Deo Boniventura Munishi 2. Juma Abdul Japhary 3. Oscar Fanuel Joshua 4. Nadir Ally Haroub (C) 5. Pato George Ngonyani 6. Thaban Michael Kamusoko 7. Simon Happygod Msuva 8. Haruna Fadhil N… Read More
Azam Fc Yazuiwa Kuvuka Barabara Mvomero Mkoani Morogoro BARABARA ya Kijiji cha Mvomero, mkoani Morogoro ililazimika kutopitika kwa takribani dakika 15 kufuatia mashabiki wa soka wa kijiji hicho kujazana kwa wingi na kufunga barabara hiyo wakati wakiipokea Azam FC iliyotoka kuic… Read More
LIVE UPDATES KUTOKA TAIFA: YANGA vs MWADUI FC....... MANUNGU COMPLEX - MOROGORO: MTIBWA vs AZAM FC FULL TIME YANGA 2 - 1 MWADUI Msuva 3' Kelvin 13' Niyonzima 86' FULL TIME MTIB… Read More
0 comments:
Post a Comment