BEKI kisiki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, ameondoka nchini leo saa 9.35 Alasiri akielekea Afrika Kusini kwa ajili ya kutibiwa kifua ambacho kinamsumbua.
Kapombe aliyekosa mechi mbili zilizopita za Azam FC dhidi ya Toto Africans na Ndanda, alianza kuumwa na kifua wakati kikosi hicho kikijiandaa kuvaana na Toto jijini Mwanza kabla ya kukimbizwa hospitalini.
Awali beki huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kali ya mafua ambayo pia iliwaathiri baadhi ya wachezaji wa Azam FC waliotoka nchini Chad kwenye kambi ya Taifa Stars akiwemo nahodha John Bocco ‘Adebayor’ na hiyo ni kutokana na hali mbaya ya hewa iliyoko jijini N'Djamena.
Kapombe ameelekea nchini humo sambamba na Daktari wa timu, Dr. Juma Mwimbe, ambapo mara baada ya kuwasili kesho wataelekea kwenye Hospitali ya Morningside Mediclinic iliyopo jijini Johannesburg kwa ajili ya beki huyo kuanza kufanyiwa vipimo ili kubainika tatizo.
“Kapombe anasikia maumivu ya kifua na mara kwa mara amekuwa akilalamika mbavu zinamuuma, tunashukuru Mungu kwa sasa hali yake inaendelea vizuri tofauti na awali, ila tunachoenda kufanya huko ni kuangaliwa zaidi ni kinamsumbua kwa kuchukuliwa vipimo na baadaye ndio itajulikana kitaalamu ni kinamsumbua,” alisema Mwimbe wakati akizungumza na mtandao wa klabu www.azamfc.co.tz dakika chache kabla hawajaelekea huko na ndege ya Shirika la Afrika Kusini.
Beki huyo wa zamani wa Simba na AS Cannes ya Ufaransa, amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Azam FC msimu huu kwenye mechi mbalimbali alizocheza, akiwa mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 11 kwenye michuano yote, nane katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Mabao mengine mawili amefunga kwenye Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) huku moja akifunga katika Kombe la Shirikisho Afrika (CC) dhidi ya Bidvest Wits walipoichapa 3-0 jijini Johannesburg kabla ya kufuzu raundi ya pili ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 7-3 na sasa itakutana na Esperance de Tunis Jumapili ijayo (Aprili 10) na mchezo wa marudiano jijini Tunis Aprili 20.
Chanzo: Azam fc official site.
Thursday, April 7, 2016
Kapombe Akimbizwa Sauzi Kwa Matibabu
Related Posts:
Serengeti Boys Kukipiga Na Marekani na Korea Kusini Timu ya taifa ya Tanzania vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inatarajiwa kushiriki mashindano maalumu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini India, yatakayozishirikisha nchi za Marekani, Malasyia n… Read More
TFF Yasikitishwa Na Vurugu Za Mashabiki Wa Simba Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es s… Read More
Angalia Hapa Jinsi Hans Pope Alivyonusurika Kipigo Kutoka Kwa Mashabiki Wa Simba Angalia video hii hapa chini … Read More
Yanga Yapata Dawa Ya Al Ahly Mabingwa wa Tanzania mara 25 Young Africans imeondoka jumapili hii kuelekea nchini Misri kuvaana na wababe wa soka Afrika Timu ya Al Ahly Jumatano hii katika mchezo wa marudiano Klabu Bingwa Afrika hatua ya 18 bora. … Read More
Msafara Wa Yanga Wawasili Salama Nchini Misri Msafara wa Yanga umewasili salama nchini Misri. Msafara huo uliondoka jioni ya jama kuwafuata National Al Ahly katika mchezo wa marudiano klabu bingwa barani Afrika. Mchezo wa kwanza uliopigwa hapa Dar timu hizo zilitoshan… Read More
0 comments:
Post a Comment