Mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ligi kuu Tanzania bara uliowakutanisha Yanga na JKR umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi mnono wa magoli matatu kwa bila.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Michael Aidan 38' (Goli la kujifunga), na mengine yakifungwa na Simon Msuva kunako dakika za 57' na 93'
Kwa matokeo hayo Yanga inarudi kileleni katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi hiyo huku wakisubiri matokeo ya mahasimu wao klabu ya Simba inayoshuka dimbani kesho kumenyana na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Matokeo hayo ndio yataamua hatima ya Yanga kushika Usukani wa ligi au Simba kurudi katika nafasi yake iliyochukuliwa na Yanga baada ya matokeo ya Leo.
Matokeo mengine katika mechi za Leo ni:
Mwadui 1 - 0 Toto AfricansMbeya City 0 - 0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 1 - 1 Mtibwa Sugar
0 comments:
Post a Comment