Friday, June 10, 2016

URUGUAY YATUPWA NJE YA MASHINDANO COPA AMERICA 2016

Timu ya taifa ya Uruguay imetolewa rasmi katika michuano ya Copa America inayoendelea huko nchini Marekani.


Uruguay inayaaga mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha goli moja kwa bila kutoka kwa Venezuela.

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez alionekana kukerwa sana na hali hiyo hasa ukizingatia timu yake imefikia hatua ya kutolewa ikiwa yeye hajacheza mechi hata moja.

Akiwa benchi Suareza alionyesha wazi hasira zake kwa kupigapiga sehemu ambapo alikuwa amekaa. Kabla kipindi cha pili hakijaanza Suarez alionekana kupasha lakini hakupata nafasi ya kuingia uwanjani.

Kocha wa timu hiyo Oscar Tabarez alisema asingeweza kumchezesha Suarez kwa kuwa hakuwa fiti asilimia 100%.

"Mchezaji hayuko fiti kwa kucheza. Sitamchagua mchezaji ambaye hayuko fiti 100%. Alikasirika?, mimi hilo sijui. Kwangu mimi hajaniambia kitu chochote" alisema Tabarez.

Uruguay ambao ni mabingwa mara 15 wa michuano hii wa
metolewa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997.

Goli la ushindi la Venezuela lilipatikana dakika ya 36, baada ya kiungo Alejandro Guerra kupiga shuti lililopanguliwa na goli kipa na kugonga mwamba nae Solomon Rondon akaja kutupia nyavuni mpira huo.

0 comments:

Post a Comment