Thursday, April 7, 2016

Al Ahly Waanza Mbwembwe

Kocha Mholanzi wa Al Ahly ya Misri ameiongoza timu yake katika mazoezi jioni ya leo Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, lakini Waandishi wa Habari wakazuiwa kuingia.
Al Ahly waliweka walinzi wao pamoja na walinzi wa Gymkhana kuhakikisha Waandishi wa Habari hawaingii katika mazoezi hayo.
Al Ahly
Lakini kesho, klabu hiyo bora ya karne Afrika itafanya mazoezi yake Uwanja wa Taifa kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) timu wageni kuruhusiwa kufanya mazoezi Uwanja wa mechi siku moja kabla ya mechi.
Timu hiyo ya kocha Mholanzi, Maarten Cornelis Jol maarufu kama Martin Jol, kiungo wa zamani wa Bayern Munich ya Ujerumani, FC Twente ya Uholanzi, West Bromwich Albion na Coventry City za England mwenye umri wa miaka 60, iliwasili Dar es Salaam jana Alfajiri na kufikia katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Kikosi kilichotua jana chini ya kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur, Fulham za England, Hamburger SV ya Ujerumani na Ajax ya Uholanzi kinaundwa na makipa; Ahmed Abdul Monem, Mosaad Awad, Sherif Ekramy.
Mabeki; Ahmed Fathy, Bassem Ali, Mohamed Hany, Rami Rabia, Saad Samir, Ahmed Hagazy na Sabri Rahil.
Viungo; Amir El-Sulaya, Ahmed El El- Sheikh, Walid Soliman, Abdalla El Said, Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Ramadan Sobhi na Momen Zakaria.
Washambuliaji; Malick Evouna, Emad Moteab na Amr Gamal.
Yanga
Wenyeji, Yanga wameweka kambi katika hoteli ya Misali Sun Set Beach, Chake Chake kisiwani Pemba tangu Jumatatu na wanatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho.
Yanga ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm mwenye umri wa miaka 67, inatarajiwa kurejea kesho Dar es Salaam na kufikia katika hoteli moja ya kifahari ambako wataamkia kwenye mechi Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment