Leicester City ndio mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza msimu wa 2015/16, na kama inavyotegemewa na wengi kuwa idadi kubwa ya wachezaji klabuni hapo wataihama klabu hiyo tayari Kante ameshagoma kuongeza mkataba Leicester.
N'Golo Kante amegoma kuongeza mkataba Leicester City na hivyo kutoa fursa kwa Arsenal ambao wamonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo kuzidisha mbio zao za kunasa saini yake. Hadi sasa katika kikosi chote cha Leicester kilichochukua ubingwa mwaka huu N'Golo Kante ndo ameonekana kuwa mchezaji atakaekuwa wa kwanza kuondoka klabuni hapo.
Kiungo huyo Mkabaji aliyejiunga na mabingwa hao akitokea Caen ya nchini Ufaransa, amekuwa na mchango mkubwa sana katika kikosi cha Claudio Ranieri.
Kante ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka katika klabu ya Leicester kitu kinachoongeza CV yake na kumfanya aonekane mchezaji muhimu sana.
Timu ambazo zinawania saini ya Kante ni; PSG, Chelsea, Manchester City na Arsenal.
0 comments:
Post a Comment