Friday, April 8, 2016

Wadhamini Wa UEFA Kuboresha Soka La Tanzania

Shirikishio la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru kampuni ya bia ya Heineken ambao ni wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA) kwa kujitolea kufanya ukarabati wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu vilivyopo jijini Dar es salaam.

Katika barua ya Meneja Mkuu wa Heineken nchini Tanzania, Michael Mbugu kwenda kwa wakurugenzi ya Manispaa wilaya za Ilala na kinondoni, nakala yake kutumwa kwa Rais wa TFF, imeeleza mdhamini ameelekeza nguvu zake kwenye kukarabati baadhi ya viwanja nchini ili viwe katika hali nzuri na salama ili kukuza vipaji vya vijana kwenye mchezo wa soka.

Heineken imelenga kuboresha dhamira yake ya kushirikiana na jamii sehemu mbalimbali kwa kuchangia ukarabati wa viwanja vya TP Manzese kata ya Sinza, Sigara Segerea kata ya Tabata Sigara na uwanja wa Magunia Msasani uliopo kata ya Msasani.

Kufanya ukarabati wa viwanja hivyo kutatoa nafasi kwa vijana wa maeneo ya Ali Maua, Darajani, Sweet Corner na Kijiweni (uwanja wa TP Manzese), Macho, Kisiwani, Msasani na Msikitini (uwanja wa Magunia), Barakuda, Tabata, Senene, Mwembeni, Chang’ombe, Kinyerezi na Segera (uwanja wa Sigara) kufanya mazoezi na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu.

Aidha TFF inazipongeza Halmashauri za Manispaa za Ilala na Kinondoni kwa kupata nafasi ya kufanyiwa ukarabati viwanja vyao na kampuni ya Heineken, na kuziomba mamlaka hizo kuvitunza viwanja hivyo ili viweze kutumiwa na vijana wa kike na kiume katika 

0 comments:

Post a Comment