Friday, April 8, 2016

Yanga Yatakiwa Kufanya Uchaguzi Wiki Ijayo

Waziri wa Michezo Mh. Nape Kushoto

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeandikia barua klabu ya Yanga kuiagiza iwe imekwishafanya uchaguzi wake hadi kufika Aprili 15, mwaka huu.
Yanga imekwishapokea barua hiyo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakisistizwa hilo ni agizo la Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye.
Pamoja na kwamba wapo kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho dhidi ya Al Ahly, lakini tayari Yanga wameanza kulifanyia kazi agizo la Serikali na wakati wowote wanaweza kutangaza uchaguzi.
Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji Kushoto akiwa na Msaidizi wake Clement Sanga
Lakini kuna wasiwasi kama uchaguzi unaweza kuwa umefanyika hadi Aprili 15, kwa sababu muda waliopewa ni mfupi mno kukamilisha taratibu.
Yanga inapaswa kuutangaza japo kwa wiki moja uchaguzi, kugawa fomu kwa wagombea japo kwa wiki moja pia, na baada ya hapo ipatikane angalau wiki moja nyingine kwa ajili ya usaili, mapingamizi kabla ya kupiga kura kuchagua viongozi.
Yanga kwa sasa ipo chini ya uongozi ambao umekwishamaliza muda wake, chini ya Mwenyekiti Yussuf Manji na Makamu, Clement Sanga. 
Manji na Sanga waliingia madarakani Julai 15, mwaka 2012 katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za viongozi waliojiuzulu akiwemo Mwenyekiti Wakili Lloyd Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha.
Walichaguliwa pamoja na Wajumbe Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na Geroge Manyama ambao waliungana na Wajumbe waliobaki, akiwemo Salum Rupia na Mohammed Binda.
Hata hivyo, baada ya uongozi huo kumaliza muda wake mwaka 2014, Manji akaunda Kamati ya Muda, yeye na Sanga wakiendelea na nyadhifa zao.

Related Posts:

  • Misri Waihofia Stars AFCON Timu ya taifa ya Misri katika kile kinachoonekana kupania kuiondoa Taifa Stars katika michuano ya kufuzu mashindano ya Afcon 2017, wapo nchini kuifuatilia Stars kila hatua. Taarifa zinasema Meneja wa Timu hiyo yupo nchi… Read More
  • Azam Fc Kuifuata Esperance De Tunis KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kuondoka leo kuelekea jijini Tunis kwa ajili ya kukabiliana na Esperance ya huko kwenye mchezo wa marudiano wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika utaka… Read More
  • Tambwe Amechuja Awekwe Benchi Mashabiki wa Klabu ya Dar Young Africans wameonyesha kutokufurahishwa na kiwango kinachoonyeshwa na mshambuliaji wao Amis Tambwe siku za hivi karibuni. Tambwe ambe ana magoli 18 katika orodha ya wafungaji bora msimu huu an… Read More
  • Simba Nayo Sasa Ni Ya Kimataifa Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 20… Read More
  • Hiki Ndio Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi Ya Mtibwa Sugar LIGI KUU || TZ - BARA || 2015~2016. YANGA SC Vs MTIBWA SUGAR FC. UWANJA - Uwanja wa Taifa. Muda - saa 10 : 00Alasiri. >>>>>>KIKOSI CHA YANGA LEO<<<<<<<< 1. Deogratias Bonave… Read More

0 comments:

Post a Comment