Tuesday, March 7, 2017

Ratiba robo fainali Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)



Ratiba hiyo iliyotelewa mapema leo imepangwa kama ifuatvyo:

March 18 Madini fc wataikaribisha Simba Sc katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha, siku hiyohiyo ya Tarehe march 18 Kagera Sugar itaialika Mbao ndani ya Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Michezo miwili iliyobaki ni kati ya Azam FC watakapoikaribisha Ndanda fc toka Mtwara katika dimba la chamanzi.

Yanga wataikaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Michezo kati ya Azam na Ndanda, Yanga na Prisons haijapangiwa ni lini itafanyika Kutokana na Yanga kushiriki michuano ya kilabu bingwa barani Afrika huku Azam wao wakishiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.


Mshindi wa michuano hiyo kikanuni anatarajia kujishindia kombe pamoja na kitita cha Sh. milioni 50 na kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Madini vs Simba 
Kagera vs Mbao
Yanga vs Prisons
Azam vs Ndanda

0 comments:

Post a Comment