Wednesday, March 15, 2017

Azam yaifuata Mbabane Swallows kwa matumaini kibao



Timu ya Azam leo Asbuhi imeondoka Kuelekea Swaziland tayari kwa mchezo wa marudiano na  Mbabane Swallows.

Katika mchezo uliofanyika Tarehe 12 uwanja wa Chamanzi Azam waliibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 kwa goli la Ramadhani Singano.

Azam wanaenda Swaziland kutafuta sare au ushindi wa aina yoyote ile ili waweze kusonga mbele katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Mchezo huo wa marudiano utafanyika jumapili ya 19 katika Uwanja wa Somhlolo, mjini Mbabane.
Kocha Msaidizi wa timu ya Azam amewaondoa hofu watanzania kwa kusema yafuatayo ““Maandalizi yako vizuri vijana wote wanafuraha, wanaari na morali ya kuhahakisha tunasonga mbele katika raundi inayofuata, tunaenda na changamoto kadhaa, ya kwanza kuhahakisha wavu wetu hautikiswi, kama hatufungi basi tusifungwe,”.

Cheche aliendelea kusema “Tutaenda kufanya kazi ya uhakika, lakini huku nyumbani tunawaomba Watanzania watuombee dua na vilevile waendelee kutusapoti na sisi tutahakikisha tunawawakilisha vema ili kuipa hadhi nchi yetu,”

Mungu ibariki Azam

Mungu ibariki Tanzania

0 comments:

Post a Comment