Tuesday, June 28, 2016

YANGA KULIPA ZAIDI YA MILION 500 CAF

Klabu ya Yanga imetakiwa kulipa fidia ya Tsh. milioni 530 kama fidia ya gharama za mchezo wao dhidi ya TP Mazembe baada ya kuruhusu mashabiki kuingia bure uwanjani.

CAF na TFF imefikia hatua hiyo baada ya Yanga kufuta kiingilio katika mchezo wao dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa leo jioni katika uwanja wa taifa jijini Daresalaam.

Hayo yameamuliwa katika kikao kilichofanyika jana kwenye hoteli ya Coral Beach jijini Dar ambapo Maofisa wa CAF walikutana na wa TFF, Polisi,Wizara ya Habari utamaduni na michezo pamoja na viongozi wa Yanga wakiongozwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdetit.

Katika fedha hizo Asilimia 15 zinaenda CAF, asilimia 15 zingine ni gharama ya uwanja, asilimia 5 TFF, asilimia 10 baraza la michezo (BMT) wakati chama cha soka jijini Daresalaam kinapta asilimia 5.

"Watanzania waingie bure, hawajatushirikisha, sisi kama Yanga tulipenda TFF na Azam wangekaa na Yanga kupanga mchezo huu, lakini wao wamekaa wenyewe na mara kwa mara wanapenda kutoa maagizo" alisema makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akionyesha kukerwa kwake na kitendo cha TFF na Azam kukubaliana mechi hiyo irushwe bila kuwashirikisha Yanga wenyewe.

"Wadhamini wetu tungependa waone uwanja utakavyojaa, tuna mpango wa kuingia mkataba na mdhamini mpya" aliongeza Sanga.

Makamu huyo alisema kama kulikuwa na ulazima wa mchezo huo kurushwa moja kwa moja basi TFF na Yanga pamoja na Azam wangekutana kwa pamoja wakaangalia wananufaika vipi na suala hilo, ili ingewezekana basi wazime matangazo yao kwa mkoa ambao mechi inachezwa ili watu wa nje ya mkoa ndio waweze kuutazama" aliongeza Sanga

Hata hivyo Yanga imeomba wapunguziwe kiasi hicho cha fedha kwa kile walichodai kuwa lengo la kuruhusu mashabiki kuingia bure ni kutaka kumwonyesha mdhamini wao mpya ambapo wanataka kumwonyesha faida ambazo anaweza kupata akiingia mkataba na klabu ya Yanga.

Yanga ilikuwa imeshachapisha tiketi 31000 ambazo zingeuzwa kwa sh. 7000 na zingeingiza sh. 217,00,000 wakati zile za sh. 25000 zilichapishwa 8200 ambazo zingeingiza sh. milioni 205 huku VIP zilikuwa tiketi 5000 ambazo zingeingiza shi milioni 150 ambapo jumla ya fedha zote ni sh. milioni 572.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

0 comments:

Post a Comment