Tuesday, June 28, 2016

SERENGETI BOYS KUWEKA KAMBI MADAGASCAR

Timu ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" imeahidiwa kuweka kambi nchini Madagascar iwapo itaitoa Shelisheli katika mchezo wa marudiano.

Rais wa shirikosho la Soka Tanzania (TFF), Jamali Malinz  ameiahidi timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys kuweka kambi nchini Madagascar endapo itaitoa timu ya taifa ya vijana ya Shelisheli katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2017.
Ahadi hiyo ilitolewa juzi na rais huyo baada ya Serengeti boys kuichakaza Shelisheli kwa jumla ya magoli matatu kwa sufuri.

Kocha wa timu hiyo Bakari Shime amesema kambi hiyo itawasaidia vijana kuzoea mazingira ya huko kwani ndiko michuano hiyo itakakochezwa.

"Ahadi ya Malinzi ni nzuri, tumefurahi kwa sabab Madagascar ndikko michuano itafanyika kwa watakaofuzu, kwa hiyo tukizoea mazingira baadaye hatutapata shida" alisema Shime.

Malinzi aliongozana na Waziri wa Habari, sanaa na michezo, Nape Nnauye kwenye chumba cha kubadilishia nguo kwenda kuwapa pongezi vijana hao kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

0 comments:

Post a Comment