Monday, March 13, 2017

Chelsea vs Manchester United, historia na utabiri na vikosi vya leo





Chelsea na Manchester tangu mwaka 2007 wamekutana mara 3 katika michuano ya kombe la FA na Chelsea kushinda mara 2 na kutoka sare mara 1.
 19 May 2007  timu hizi mbili zilikutana katika mchezo wa fainali kombe la FA katika dimba la
Wembley na Chelsea kutwaa kombe hilo kwa kuifunga  Manchester United goli 1 kwa 0 goli la Didier Drogba            katika dakika ya 116.

Goli hilo Drogber alilifunga baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira ulipigwa na Frank Lampard na kumshinda mlinda mlango wa Manchester Edwin Van Der Sar.
Ikumbukwe Uwanja wa Wembley ndio ilikuwa mara ya kwanza kuchezewa fainali za FA hivyo Chelsea kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa katika dimba hilo ikishuhudiwa na Washabiki 89,826.
Tarehe 10 Mar 2013 timu hizo zilikutana katika Uwanja wa Old Trafford huku Washabiki 75,196 wakiwa uwanjani, timu hizo zilitoka sare ya 2 – 2 katika mchezo wa raundi ya 6.
Magoli ya Manchester yalifungwa na Javier Hernandez dakika ya 5 na Wayne Rooney dakika ya 11,

magoli ya Chelsea katika mchezo huo yalifungwa na Eden Hazard dakika ya 59, Ramires dakika 68.
Mwaka  huo huo walirudiana Tarehe 1 Apr na Chelsea walifanikiwa kuingia raundi ya 5 baada ya kuifunga Manchester goli 1 kwa 0 katika dimba la Demba Ba dakika ya 49.

Leo Chelsea v Manchester United zinakutana katika hatua ya robo fainali wakati huu ambao Chelsea inashiriki makombe mawili  EPL na FA na Manchester inashiriki makombe matatu EPL, FA na Europa na tayari wamehifadhi kombe moja.


Habari njema kwa Chelsea ni kuwa wachezaji wake 99% wako salama na hivyo wako katika ari nzuri ya kushinda mchezo wa leo ukilinganisha na Manchester ambayo wachezaji wake muhimu ni majeruhi, wachezaji majeruhi ni Wayne Rooney na Anthony Martial wakati  Marcus Rashford akiwa ana ugua. Zlatan Ibrahimovic yeyeamepewa adhabu na chama cha soka nchini Uingereza.

0 comments:

Post a Comment