Wednesday, March 15, 2017

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) limezifungia Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)




TRA yafunga ofisi za Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kwa kushindwa kutimiza mkataba
Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA bwana Richard Kayombo ndie alithibitisha hilo.

“Ni kweli tumezifunga na hiyo ni hatua ya mwisho kwetu kufanya hivyo. Tulikubaliana kulipa tunachowadai na muda umepita,” alisema.

TRA wametumia kampuni ya udalali iitwayo YONO Auction.
YONO iliwaamuru wafanyakazi hao kuacha kila kitu.
TRA inawadai TFF mapato kutoka kwa kocha mkuu wa zamani wa Tanzania na kodi ya mchezo kati ya Tanzania na Brazil.

0 comments:

Post a Comment