Baada ya jana ijumaa timu ya azam kuibuka na ushindi ugenini
wa goli 3 – 2 dhidi ya wenyeji wao Kagera sugar na kufufua matumain ya kuwania
kombe la Vodacom baada ya kufikisha pointi19 nyuma ya stand utd, Yanga na
simba.
Leo jumamosi na kesho jumapili ligi hiyo itaendelea katika
nyasi za viwanja mbalimbali kama ifuatavyo
Huko jijini Mbeya wenyeji Mbeya City wataikaribisha timu
inayokuja kwa kasi kutoka chini baada ya kubadili kocha na kumrudisha Kali
Ongala Majimaji ya Songea katika dimba la Sokoine.
Mchezo mwingine ni kati ya wenyeji Toto Africans dhidi ya
Mtibwa Sugar ya Morogoro katika dimba la CCM Kirumba.
Mchezo unaosubiriwa kwa hamu ni kati ya vinara wa ligi hiyo
Simba watakapokuwa wageni wa timu ya Mwadui FC ya Shyinyanga, katika dimba la
CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Africans Lyon itakua mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye
uwanja wa Uhuru,
Mchezo wa mwisho siku ya leo ni kati ya JKT Ruvu ya Pwani na
Ndanda FC ya mkoani Mtwara katika dimba la Mabatini mkoani Pwani.
Kesho jumapili Mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakiwa na
furaha baada ya kurudi kwa kocha wao mkuu watashuka uwanja wa Uhuru
kuikaribisha timu iliyopanda daraja kutoka Mwanza timu ya Mbao FC, Wakati huko
Mkoani Pwani wenyeji Ruvu Shooting Star itakapoikaribisha timu yaStand United
ya Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment