Friday, May 20, 2016

SALUM MAYANGA HUYU NI CLAUDIO RANIERI WA LIGI KUU BARA

Kutoka Katika kupigania kutoshuka Daraja Msimu wa 2014/15 Hadi Kushika Nafasi Ya 4 Katika Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu Wa 2015/16, Ni Dhahiri kuwa Mayanga Ni Bonge La Kocha.

Salum Mayanga

Itakumbukwa kuwa msimu wa 2014/2015 Timu Ya Tanzania Prisons ilikuwa katika hatari ya kushuka Daraja kutokana na kuwa na msimu mbovu hadi alipotokea kocha Mbwana Makata akainusuru timu hiyo kutokushuka Daraja, Kutokana na kuisadia timu ya Prisons Makata alipewa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa ligi kuu.

Katika Msimu huu unaomalizika Mei 22 Tanzania Prisons imeshajihakikishia usalama wa kubaki katika Ligi na sasa inashika nafasi ya 4 huku ikizidiwa pointi moja tu na Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya 3. Ujio wa Mayanga katika kikosi cha Tanzania Prisons umekuwa na faida kubwa na mwendelezo mzuri wa ukuaji wa soka katika klabu hiyo, Mayanga amefanya kazi kubwa na nzuri katika kuimarisha kikosi cha Prisons, Ameimarisha Safu ya Ulinzi ikiongozwa na Mlinda Mlango Ben Kakolaki, katika michezo 29 waliyocheza katika ligi wameruhusu kufungwa magoli 22 tu, hivyo kuifanya kuwa timu ya tatu katika orodha ya timu zilizoruhusu magoli machache baada ya Yanga na Simba.

Ubora wa kikosi cha Prisons pia umedhihirika si tu kwa timu za hadhi yake bali hata kwa timu zote kubwa katika ligi kuu msimu huu zikiwemo Yanga, Azam FC na Simba kwani timu hizi 3 zote zimeshindwa kutokana na alama 3 katika Dimba la Sokoine Jijini Mbeya. Mayanga pia amesuka safu nzuri ya ushambuliajia, Jeremiah Juma na Mkopi wamefanya kazi kubwa sana katika kuifikisha Prisons hapa ilipo kwa sasa kutokana na kazi nzuri ya Mayanga,Jeremiah amefikisha idadi ya magoli 13 katika ligi kitu kinachomfanya kuwa miongoni mwa waliofunga idadi kubwa ya magoli katika msimu huu.

Timu nyingi za Ligi kuu Bara zinaharibika na kupotea kwa sababu ya migogoro isiyonafaida, Prisons ni wakati wao wa kukaa na kudumisha umoja na kumpa nafasi zaidi Mayanga kuonyesha uwezo wake.

0 comments:

Post a Comment