Tottenham Jana ilisafiri kuifuata Chelsea katika dimba la Stamford bridge, kabla ya mchezo huo wa jana Tottenham ilikuwa haijawahi kuifunga Chelsea katika uwanja huo kwa takribani miaka 23, Mameneja 17 wamesajiliwa na kuachwa na klabu ya Tottenham lakini hakuna aliefanikiwa kuwafunga The Blues katika uwanja wao wa nyumbani, Jana ilikuwa ni mara yao ya 26 wanakutana tangu Feb. 10, 1990 ambapo Tottenhama waliifunga Chelsea Stamford Bridge kwa mara ya mwisho, na katika mara hizo 26, Chelsea wameshinda mara 16, mara 10 wakitoa sare. Wakati huo Tottenham wanaifunga Chelsea katika Dimba la Stamford Bridge,Gareth Bale alikuwa na umri wa Miezi 6 tu.
Hali hiyo imeendelea tena jana baada ya Tottenham kushindwa kumaliza ukame huo wa miaka 23 mfululizo katika dimba hilo la Chelsea, Wao ndo walikuwa wa kwanza kupata magoli yote mawili yaliyofunga na Kane dakika ya 35 na Son dakika ya 44, Chelsea walijipanga vizuri na waliporudi katika kipindi cha pili walisawazisha magoli hayo yote kupitia kwa Garry Cahil dakika ya 58 na Eden Hazard dakika ya 83.
Matokeo hayo yamekuwa ni furaha kubwa kwa wachezaji na mashabiki wa Leicester City ambao kwa sasa wanakuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo msimu huu.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment