Mshambuliaji hatari wa Real Madrid Christiano Ronaldo yupo fiti kuivaa Manchester
City Jumatano hii katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya Klabu
bingwa Ulaya.
Ronaldo wiki iliyopita alimaliza mchezo wa kwanza wa
nusu fainali bila kufunga goli katika uwanja wa Etihad huku akitoka na maumivu
ya mguu, maumivu ambayo yalimuweka nje pia katika mchezo wa La Liga dhidi ya
Real Sociedad ambapo Madrid ilishinda kwa goli 1 – 0, hata hivyo kapteni huyo
wa timu ya Taifa ya Ureno ameshiriki katika mazoezi ya timu na wachezaji
wenzie.
Wakati taarifa za Ronaldo zikionyesha wazi kuwa atauwahi
mchezo huo, hali iko tofauti kwa Karim Benzema ambae haijafahamika kama
atacheza katika mchezo huo dhidi ya Man City.
Karim Benzema alitolewa wakati wa mapumziko katika mchezo waliocheza dhidi ya
Man City kutokana na kupata maumivu ya misuli.
0 comments:
Post a Comment