Sunday, April 24, 2016

Leicester City Yazidi Kupaa Kileleni Wakati Arsenal Ikivutwa Shati


Timu inayoishangaza dunia msimu huu katika ligi kuu ya Uingereza Leicester City imezidi kulisogelea taji la EPL baada ya kutoa kichapo kikali kwa Swansea.

Leicester City ambayo leo imecheza huku ikimkosa mshambuliaji wake hatari Jamie Vardy imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4 - 0 dhidi ya Swansea. Magoli ya Leicester yamefunga na R. Mahrez dakika ya 10', L. Ulloa dakika ya 30' na 60' huku lile la nne likifungwa na M Albrighton dakika ya 85' ya mchezo. kwa matokeo haya Leicester wanafikisha jumla ya pointi 76 wakiwa wamecheza mechi 35, wakifuatiwa na Tottenham wenye pointi 68 katika mechi 34 walizocheza.



Nao Arsenal walishuka tena dimbani leo kucheza na Sunderland na mechi hiyo kuisha kwa suluhu ya bila kufungana, matokeo hayo yanaiacha Arsenal katika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 64 na michezo 35.












pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment