Sunday, April 24, 2016

Azam FC Yatinga Fainali Kombe La FA


Azam Fc imetinga hatua ya fainali ya kombe la shirikisho baada  ya kuiondosha Mwadui Fc kwa mikwaju ya penati 5-3. Mechi hiyo ambayo ilikuwa na kasi na ushindani mkubwa ilimalizika kwa sare ya 1 - 1 katika dakika 90 za kawaida, katika dakika 30 za nyongeza Azam Fc walifanikiwa kupata goli la pili dakika ya 96 kupitia kwa Bocco.
Mwadui walisawazisha goli hilo dakika ya 120 kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa azam kunawa katika eneo la penati box.
Hata hivyo Mchezaji mmoja wa Mwadui alipoteza penati moja Huku Azam wao wakifunga penati zote Tano.
Azam FC sasa hivi wanasubiri hatima ya mechi kati ya Coastal Union na Yanga SC iliyovunjika kutokana na vurugu zilizosababishwa na mashabiki wa Coastal Union ili wajue nani wanacheza nae katika hatua ya fainali.






pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment