Sunday, April 24, 2016

BREAKING NEWS: Mechi Kati Ya Coastal Na Yanga Yavunjika


Mechi kati ya Coastal na Yanga imevunjika baada ya vurugu zilizoanzishwa na mashabiki wa Coastal Union Baada ya Yanga kuongeza goli la pili katika dakika 30 za nyongeza goli lililofungwa na Hamisi Tambwe dakika ya 100 ya Mchezo.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa mashindano hayo Jemedali Saidi, Hatima ya mechi hiyo inasubiri ripoti ya Kamisaa pamoja na Mwamuzi wa mchezo huo ili kuiwezesha kamati ya mashindano kukaa na kuamua nini kitafanyika kuhusu mchezo huo.

Vurugu hizo zilianza kidogokidogo baada ya Yanga kusawazisha goli dakika ya 60 kupitia kwa Donald Ngoma goli ambalo lililalamikiwa na Coastal kuwa ni Offside, lakini baada ya goli la pili la Yanga ndipo mashabiki wa Coastal wakaanza kurusha mawe uwanjani hasa upande wa lango la Yanga alikokasimama Deogratius Munish mlinda mlango wa Yanga, Vurugu hizo zilichochewa pia na kadi nyekundu aliyopewa beki wa Coastal baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Yanga.





pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment