Friday, May 13, 2016

KAMPENI KUTETEA KAGAME CUP AZAM FC NI JULAI 16


Timu ya Azam FC, itaanza kutetea ubingwa wake wa Kombe la Kagame kuanzia Julai 16 hadi 30 mwaka huu, michuano ambayo itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Hii inakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa michuano hiyo kufanyika Dar es Salaam,mwaka jana Azam FC iliutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Gor Mahia ya nchini Kenya kwa mabao 2-0.

Uongozi wa Azam FC umepokea barua rasmi kutoka TFF, waandaaji kwa mara nyingine wa michuano hiyo, barua inayoeleza ufanyikaji wa michuano hiyo, ambayo awali ilipangwa kupigwa visiwani Zanzibar.

Azam FC iliweza kuifikia rekodi ya klabu kongwe ya SC Villa ya Uganda waliyoiweka mwaka 2005 baada ya kutwaa ubingwa huo kwa staili ya kipekee kwa kushinda mechi zote na kutofungwa bao lolote ndani ya dakika 90.

0 comments:

Post a Comment