Sunday, May 15, 2016

LEWANDOWSKI AIFIKIA REKODI ILIYOWEKWA MIAKA 39 ILIYOPITA


MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Borrusia Dortmund anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich kwa sasa Robert Lewandowski amefikia rekodi iliyowekwa miaka 39 iliyopita katika ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Robert Lewandowski amethibitisha ubora wake katika ligi ya Ujerumani Bungesliga akifanikiwa kufunga magoli 30 baada ya mchezo ambao Bayern walicheza na Hannover siku ya jumamosi na kuibuka na ushindi wa magoli 3 - 1.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland amempiku staa wa Dortmund Pierre-emerick Aubameyang katika mbio za kuwania tuzo ya mfungaji bora wa ligi kwa kufikisha magoli 30 akifikia pia rekodi iliyowekwa mwaka 1977 ya mchezaji asiye Mjerumani kufikisha idadi ya magoli 30 katika msimu mmoja wa ligi kuu nchini Ujerumani,  huku Aubameyang akiwa na magoli 25.
Koln’s Dieter Muller alilkuwa mchezaji wa mwisho kufikisha idadi ya magoli 30 akifunga magoli 34 katika msimu wa 1976/77 huku timu yake ikimaliza katika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi

Gerd Muller yeye ndo anashikilia rekodi ya ufungaji katika ligi ya Ujerumani akifanikiwa kufunga jumla ya magoli 40 katika msimu mmoja.

0 comments:

Post a Comment