Mchakato wa Azam Fc kusaka mchezaji bora wa timu hiyo umemalizika hivi karibuni na Shomari Kapombe kuibuka mshindi wa tuzo hizo.
Azam Fc imetoa tuzo kwa wachezaji wake wanne waliopata kura nyingi kutokana na msaada wao katika timu hiyo uliousaidia Azam Fc kumaliza katika nafasi ya pili ligi kuu Vodacom msimu wa 2015/16.
Shomari Kapombe ndiye aliyeibuka kinara kwa kujikusanyia kura 277 akifuatiwa na kipa Aishi Manula aliyepata kura 120, Pascal Wawa nafasi ya tatu kwa kura 40 na nafasi ya nne imeenda kwa kiungo mkabaji Himid Mao aliyejipatia kura 30.
Mtendaji mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema huo ni utaratibu ambao wamejiwekea kwa lengo la kuwaongezea hamasa ya kujituma wachezaji wao ili kuongeza ushindani na kupata mafanikio.
"Tutatoa zawadi kwa kila mshindi zawadi ambayo itakuwa kubwa lengo ni kuamsha ari na kuongeza ushindani kwa wachezaji wetu ili tuweze kufanya vizuri katika mashindano tunayoshiriki" alisema Kawemba.
Monday, June 13, 2016
Home »
» SHOMARI KAPOMBE KINARA TUZO ZA MCHEZAJI BORA AZAM FC
0 comments:
Post a Comment