Sunday, April 10, 2016

Jose Mourinho Safari Hii Kwenye Ngumi


Nyota kibao wa soka na michezo mingine wamejitokeza kushuhudia pambano la uzito wa juu ubingwa IBF kati ya Anthony Joshua na Mmarekani Prince Martin. Joshua ameshinda pambano hilo kwa KO katika raundi ya pili.

Lakini kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho ameibukia kwenye ngumi hizo na kuendeleza vituko vyake.

Wakati Joshua akiendelea kushambulia na wengi kupata midadi kwa kusimama, Mourinho aliendelea kuketi huku ikionekana hakuwa akiona kitu kuhusiana na pambano hilo na wala hakujali huku ikionekana ni kama kitu kilichomshangaza.



0 comments:

Post a Comment