Sunday, April 10, 2016

Man Paquiao Amaliza Ubishi Wa Nani Mkali Kati Yake Na Bradely


 Man Pacquiao ameithibitishia dunia kuwa yeye ni mkali zaidi kwa kumtwanga Mmarekani Timothy Bradely katika mpambano uliofanyika katika ukumbi maarufu wa MGM Grand jijini Las Vegas.Pacquiao alishinda pambano hilo kwa pointi baada ya kumwangusha Bradely mara mbili katika raundi ya saba na raundi ya tisa.Majaji wa pambano hilo walimpa ushindi wa pointi mtailandi huyo na kumaliza ubishi wa waliokuwa wanatilia shaka uwezo wake.



Pac Man alifanikiwa kumtwisha Bradely jumla ya makonde 122 kati ya makonde 439 aliyoyarusha huku ngumi 99 kati ya 302 zilifanikiwa kuingia mwilini mwa Pac Man kutoka kwa Mmarekani Bradely.

0 comments:

Post a Comment