Tuesday, October 11, 2016

CHRISTIAN BENTEKE AWEKA REKODI YA PEKEE UBELGIJI

Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke amefunga bao la Mapema zaidi katika mechi zinazoendelea za kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Gibraltar lililopatikana katika sekunde ya 8.1 ya mchezo huo.

Benteke, anayeitumikia klabu ya Crystal Palace ya nchini Uingereza alifunga mabao matatu wakati wa mechi hiyo ya Kundi H ambayo Ubelgiji walishinda 6-0.
Wafungaji wengine walikuwa ni Eden Hazard, Axel Witsel na  Dries Mertens.

Bao hilo la kwanza la Benteke limekuwa bao la kasi zaidi kuwahi kufungwa na mchezaji wa Ubelgiji.
Benteke amevunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Davide Gualtieri wa San Marino dhidi ya England mwaka 1993, mechi za kufuzu Kombe la Dunia,la sekunde 8.3.

Mechi zingine, Ufaransa iliibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na kiungo wa Manchester United, Paul Pogba dhidi ya Uholanzi, Sweden waliilaza Bulgaria 3-0, Ureno nao wakaishindilia Visiwa vya Faroe 6-0.
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

0 comments:

Post a Comment