Ligi kuu ya uingereza imeendelea tena leo kwa michezo sita
kupigwa katika viwanja sita tofauti
Mchezo wa mapema ulipigwa Stamford bridge pale Chelsea walipoiadhibu
bila huruma bingwa mtetezi wa ligi hiyo Leicester City kwa goli 3 bila majibu kwa magoli ya Diego costa dakika ya 7 kabla ya
Eden Harzad kufunga la pili dakika ya 33 na msumari wa mwisho ulipigiliwa na
mnigeria Victor Mosses dakika ya 80 na kuifanya Chelsea kufikisha alama 16 na
kupanda mpaka nafasi ya 5
Wakati
huohuo mambo yanaendelea kumuendea kombo Gudiola baada ya leo kukaliwa kooni na
kulazimishwa kutoka sare ya goli 1 kwa 1 na Everton, ilikua ni Everton ndio
walioanza kulifumania lango la Man city dk 64 kupitia kwa Lukaku kabla ya
Nolito kuisawazishia city katika dk 72
Stoke
city wao walitoa onyo kwa sunderland kwa kuibugiza magoli miwili kwa bila kwa
magoli ya Joe Allen dk 9 na 45 ya mchezo
Arsenal
wameendelea kutoa dozi na kuikaribia man city kileleni baada ya kuipiga kumbo
Swansea city 3 2 kwa magoli miwili ya Theo Walcot na moja la Mesut Ozil magoli
ya Swansea yalifungwa na Sigurdsson na Borjan Boston
AFC Bournemouth imefanya
kufuru kwa Hully City baada ya kupiga
goli 6 kwa 1
West Bromwich Albion
wameondoa furaha ya Tottenham Hotspur waliyokua nayo wiki moja iliyopita baada
ya kuifunga man city baada ya kugawana alama mojamoja Kutokana na sare ya 1 1
goli la Tottenham Hotspur likifungwa na Dele Alli dk 89 huku lile la mapema la West
Bromwich Albion likifungwa dk44 James mc Clean
0 comments:
Post a Comment