Kiungo wa klabu ya Manchester City, raia wa Ivory Coast Yaya Toure amesaini mkataba mpya utakaoendelea kumuweka mchezaji huyo klabuni hapo kwa mwaka mmoja zaidi.
Hatua hiyo inafikiwa baada ya Pep Guardiola kuridhika na kiwango cha mchezaji huyo achilia mbali tofauti waliwahi kuwa nazo mwanzoni kabisa mwa msimu.
Kiungo huyo 34, ambaye mkataba wake wa zamani umemalizika mwezi huu, alianza msimu uliomalizika kwa kuingia katika mtafaruku na kocha Guardiola hali iliyopelekea hadi kuondolewa katika kikosi cha Manchester City kilichoshiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya, na hatimaye Guardiola kusema kama Toure angependa kuendelea kuwepo kikosini basi alitakiwa kumuomba yeye msamaha, hali hiyo iliendelea ya Toure kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha City hadi pale ambapo Toure aliamua kuweka tofauti zake pembeni na kuomba msamaha na hatimaye kurudishwa kikosini na leo anaongezewa tena muda wa kuendelea kuitumikia City.
"Toure amekuwa mchezaji mzuri sana katika kikosi cha City na ameendelea kuwa na mchango muhimu sana katika kikosi cha Guardiola" alisema mkurugenzi wa klabu hiyo Tixiki Begiristain akiiambia Mancity.com
Kwa taarifa za papo kwa papo za Usajili na yote yanayohusu Soka, Ni hapahapa Soka24
0 comments:
Post a Comment